Loading...

HATIMAYE DIAMOND NA ALIKIBA WAWAKUNA WANASIASA- WAWILI HAO WATOA MAMILIONI KUCHANGIA JAMBO MUHIMU KATIKA MAISHA YA WATOTO KUMBE WAWILI HAO NI ZAIDI YA UNAVYOWAFAHAMU...

Mbunge wa Chalinze Mhe. Ridhawani Kikwete amewapongeza wasanii wa muziki, Diamond Platnumz na AliKiba kwa kutoa msaada wa tsh 41milioni kwa ‘GSM Foundation’ ili kusaidia jitihada za taasisi hiyo za upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi.
Diamond na Ali Kiba

Mtoto huyo wa Rais mtaafu, amewapongeza wasanii hao kwa kuonyesha kuguswa na kusaidia matatizo ambayo yanatokea katika jamii.

“Katika vitu vimeonyesha umuhimu wa kuwa stars katika jamii yetu ni hili mlilolifanya wadogo zangu. Ni jambo la kusifiwa na Mungu atawalipa kwa kuwaongezea maarifa ya kufanya kazi zenu vizuri,” Ridhiwani aliandika katika instagram yake.

Aliongeza, “Pia niwapongeze sana GSM Foundation kwa kazi nzuri mnayoifanya. Kutoa si utajiri, ni moyo na mungu atakuzidishia ndugu mkurugenzi Gharib pale ulipotoa. Kila la kheri katika kusaidia jamii yetu yenye mahitaji. Peace to you,”

Siku chache zilizopita Diamond Platnumz alitoa msaada kwa taasisi hiyo wa tsh 20 Milioni na baadae AliKiba na yeye aliamua kutoa tsh 21 Milioni.

http://www.udakuspecially.com/2016/08/ridhiwani-kikwete-awapongeza-alikiba-na.html

UKWELI WOOTE HUU HAPA: DIAMOND AFUNGUKA NA KUKIRI KUWA NI KWELI KWAMBA YEYE HUPENDA MAMBO HAYA TAZAMA ORODHA YA MAMBO HAYO HAPA...

 

Msanii Diamond Plutnuz amewashangaza watu baada ya kauli yake kwamba anaona bifu kwenye muziki na kitu kizuri, tofauti na wasanii wenzake wengi ambao hupinga suala la bifu.


Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Diamond amesema kwake yeye anaona ni sawa tu iwapo wasanii wanakuwa na bifu, kwani inasaidia kwa kiasi kikubwa kuinua muziki wao, kwa kuzungumziwa na vyombo vya habari na watu mbali mbali, isipokuwa inakuwa shubiri pale inapogusa familia, na kutoleana maneno machafu.

“Bifu mi naona fresh, kwangu kitu kikizungumziwa ndo naona poa tu kwanza inaniongezea, ila pale inapofikia kugusa kwenye familia na kutoleana maneno machafu ndio inakuwa sio poa”, alisema Diamond Plutnumz.

Kutokana na kauli hiyo, Diamond amekuwa amepigia mstari kuwa wasanii wa lebo yake ya WCB hutegemea ‘kiki’ zaidi kuliko kazi bora kuweza ku-hit, kama ambvyo watu wengi huwatuhumu wasanii hao.

Pia Diamond ametoa siri kuwa mashabiki wake wajiandae mkao wa kula kwani kabla mwaka huu kuisha, atatoa album ambayo itakuwa ya kimataifa.
Chanzo
http://www.udakuspecially.com/2016/08/diamond-akiri-kupenda-bifu.html
Older Posts
© Copyright Amour | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top