Akizungumza kwenye ofisi ndogo ya CCM jijini Dar es salaam leo akitokea mkoani Mwanza Rais Magufuli amesema kwamba mpango wa serikali kuhamia Dodoma uko pale pale ikiwa ni ahadi yake mara baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CCM mkoani Dodoma mwezi uliopita.
Rais Magufuli alisema serikali pamoja na watumishi wote wa watahamia Dodoma ila Ikulu ya Rais jijini Dar es salaam itabaki kama Makumbusho.
“Hatuwezi kuuza ikulu, Ikulu itabaki pale kama makumbusho” Alisema Rais Magufuli huku akishangiliwa na baadhi ya wanachama chama cha Mapinduzi.
Naye Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amemhakikishia Rais kuwa watatekeleza kwa ukamilifu maagizo yake ikiwa na pamoja na Mpango wa serikali kuhamia Dodoma.
Kwa upande mwingine Rais Dkt. John Magufuli hivi karibuni alitangaza kuuza majengo ya wizara Dar es Salaam, atakapohamia yeye katika makao makuu ya nchi mkoani Dodoma.
Rais Magufuli alisema hayo hivi karibuni kwenye mkutano wa hadhara mkoani Singida, katika siku ya kwanza ya ziara yake ambapo alisisitiza kuwa atahakikisha anauza baadhi ya majengo hayo kwa mnada, ili wale wasiotaka kuhama, wahame kwa lazima.
chanzo:
http://www.udakuspecially.com/2016/08/rais-magufuli-ikulu-ya-magogoni.html
Post a Comment