Loading...

HAYA N'DO MAMBO YA MAANA SASA: SERIKALI YAPIGA MARUFUKU MASHINDANO YA WENYE MAKALIO MAKUBWA

Serikali ya Burkina Faso imepiga marufu shindano ya kila mwaka kwa wanawake wene makalio makubwa kwa maelezo kuwa shindano hilo halina maadili na linaleta ubaguzi katika jamii.

Tangazo la shindano hilo maarufu kama “Miss Bim-Bim” lililoonyesha wanawake wawili wenye makalio makubwa sana, lilizungua maswali mengi kwenye mitandao ya kijamii nchini humo.

Baada ya watu kukosoa tamasha hilo, Waziri mwenye dhamana, Laure Zongo alisema kazi ya serikali ni kuhakikisha kuwa mwanamke hanyanyaswi na kuwa maoni ya watu kwenye mitandao ya kijamii imemsukuma kuzungumzia tukio hilo.

Mtayarishaji wa mashindani hayo, Hamado Doambahe alisema kuwa walikuwa na lengo la kusifia umbo zuri la mwanamke wa ki-Afrika na wala sio kulenga kufanya jambo lolote baya.

Mashindano ya namna hii yamekuwa yakifanyika katika nchi nyingine Magharibi mwa Afrika na kuwa wanawake wamekuwa na mitazamo tofauti juu ya mashindano haya.
http://www.udakuspecially.com/2016/08/serikali-yapiga-marufuku-mashindano-ya.html

Post a Comment

CodeNirvana
Older Posts
© Copyright Amour | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top